Our Loans GreenPath Loan Product

Personalized Loan

A quick personal financing solution designed to support short-term needs such as school fees, household expenses, and urgent priorities.

Walengwa

Nani anaweza kuomba?

Wafanyakazi wenye mikataba maalumu ambao wanaweza kupata udhamini wa kazi kutegemeana na net ya mshahara, net kuanzia shilingi 600,000 au udhamini wa mtu mwingine yeyote anayekidhi vigezo vya udhamini.

Viwango vya MkopoTZS 1M - TZS 10M
Lengo la MkopoMahitaji mbalimbali ya kibinafsi na ya kimaendeleo kama vile kulipia kodi za nyumba, ada za shule, uwekezaji, na mahitaji mengine ya haraka.
Muda wa MkopoSio zaidi ya miezi 12
RejeshoKila mwezi
Sifa

Mkopo huu umeundwa kwa wafanyakazi na wateja wenye kipato kinachothibitika wanaohitaji ufumbuzi wa haraka na unaopimika.

  • Kiasi cha mkopo kuanzia TZS 1M hadi TZS 10M kulingana na uwezo wa marejesho
  • Tathmini ya awali hufanyika haraka baada ya nyaraka kukamilika
  • Marejesho ya kila mwezi yanayolingana na mzunguko wa mshahara
  • Inaweza kutumia udhamini wa kazi, mdhamini, au dhamana inayokubalika
  • Inafaa kwa mahitaji binafsi, familia, elimu, kodi, na maendeleo
Faida
  • Inasaidia kutatua mahitaji ya haraka bila kuvuruga mipango yako ya muda mrefu
  • Unapata mwongozo wa tawi kuhusu kiasi kinachofaa na ratiba ya marejesho
  • Mchakato wa awali wa mtandaoni hupunguza muda wa kuanza maombi
  • Inaweka uwazi kwenye gharama, nyaraka, na dhamana kabla ya hatua ya mwisho
Vigezo na Mahitaji

Vigezo muhimu

  • Net ya mshahara kuanzia TZS 600,000 au mdhamini anayekidhi vigezo
  • Mkataba wa kazi, kitambulisho cha kazi, na barua ya utambulisho kutoka kwa mwajiri
  • Salary slip za miezi 3 na bank statement ya miezi 6 ya hivi karibuni
  • Dhamana kama gari, nyumba, kiwanja, au mdhamini pale inapohitajika
  • Ombi lililojazwa kikamilifu na utambulisho wa Serikali za mtaa

Dhamana na gharama

  • Usajili wa mkopo
  • Tunakopea 3rd party dhamana kutoka kwa mdhamini wako pia
  • Ada ya kuratibu mkopo ni 3% inayolipwa wakati wa kuchukua mkopo
  • Gari iliyopo katika ubora unaoridhisha na ina bima kubwa
  • Nyumba/kiwanja kilichoendelezwa na zenye hati rasmi
  • Ufungaji wa Car Track pale gari linapotumika kama dhamana

Viambatanisho

  • Ombi la mkopo lililojazwa kikamilifu
  • Utambulisho wa Serikali za mtaa
  • Picha moja ya muombaji
  • Kitambulisho cha kazi
  • Mkataba wa kazi (Employment Contract)
  • Barua ya utambulisho kutoka kwa mwajiri wako (Introduction Letter)
  • Mdhamini wa mkopo
  • Shahada za mshahara (Salary Slip) za miezi 3 ya hivi karibuni
  • Bank statement ya miezi 6 ambako mshahara wako unapitia
  • Picha ya dhamana
Maswali

Maswali kuhusu Personalized Loan

Nani anaweza kuomba Personalized Loan?

Mfanyakazi mwenye mkataba, kipato kinachothibitika, au muombaji mwenye mdhamini anayekidhi vigezo anaweza kuanza maombi.

Ninaweza kupata mkopo ndani ya saa 48?

Ndani ya saa 48 ni lengo la tathmini ya awali baada ya taarifa na nyaraka muhimu kukamilika. Uidhinishaji hutegemea uhakiki wa mwisho.

Je, lazima niwe na dhamana?

Dhamana au mdhamini anaweza kuhitajika kulingana na kiasi cha mkopo, kipato, na tathmini ya hatari.

Nitatumia mkopo huu kwa nini?

Unaweza kutumia kwa ada, kodi, mahitaji ya familia, uwekezaji mdogo, matibabu, au mahitaji mengine ya maendeleo.

Ready to apply?

Anza maombi ya Personalized Loan sasa.

Jaza fomu fupi ya mtandaoni kwa taarifa zako na kiasi unachohitaji. Timu ya GreenPath itawasiliana nawe kuthibitisha nyaraka, kutathmini uwezo wa marejesho, na kukuongoza katika hatua zinazofuata.

Anza maombi