Our Loans GreenPath Loan Product

Tender Loan

Project and tender financing designed to support timely completion of ongoing work, procurement needs, and contract delivery.

Walengwa

Nani anaweza kuomba?

Wakandarasi, watoa huduma, na biashara zenye tender, LPO, au mikataba inayohitaji mtaji wa utekelezaji kwa wakati.

Viwango vya MkopoKulingana na thamani ya tender/mkataba na tathmini
Lengo la MkopoKununua vifaa, kulipa gharama za utekelezaji, kuongeza mtaji wa mradi, au kukamilisha kazi kwa wakati.
Muda wa MkopoKulingana na muda wa mkataba au mradi
RejeshoKulingana na cash-flow ya mradi au malipo ya mkataba
Sifa

Tender Loan ni ufadhili wa utekelezaji wa mikataba, LPO, na miradi inayohitaji mtaji wa kununua vifaa au kukamilisha kazi kwa wakati.

  • Inalenga wakandarasi, suppliers, na biashara zenye mikataba au LPO halali
  • Tathmini hutazama thamani ya mkataba, gharama za utekelezaji, na mpango wa malipo
  • Inaweza kufadhili vifaa, kazi, usafirishaji, au gharama za mradi
  • Muda wa mkopo unaweza kuendana na muda wa mkataba au malipo ya mteja
Faida
  • Inasaidia kukamilisha kazi kwa wakati bila kukwama kwa mtaji
  • Inaweka mpango wa marejesho kulingana na cash-flow ya mradi
  • Tawi husaidia kupitia nyaraka za mradi kabla ya uamuzi
  • Inaweza kuongeza uwezo wa biashara kuchukua kazi kubwa zaidi kwa nidhamu ya fedha
Vigezo na Mahitaji

Vigezo muhimu

  • Mkataba, LPO, purchase order, au nyaraka za tender zilizothibitishwa
  • BOQ, makisio ya gharama, na mpango wa utekelezaji
  • Taarifa za benki za biashara na usajili wa kampuni au biashara
  • Dhamana inayokubalika na uthibitisho wa uwezo wa kutekeleza mradi

Dhamana na gharama

  • Mkataba, LPO, au nyaraka za tender zilizothibitishwa
  • Dhamana inayokubalika kulingana na kiasi cha mkopo
  • Uhakiki wa uwezo wa kutekeleza mradi
  • Mpango wa malipo kutoka kwa taasisi au mteja wa mradi

Viambatanisho

  • Ombi la mkopo lililojazwa kikamilifu
  • Utambulisho wa Serikali za mtaa
  • Picha moja ya muombaji
  • Kitambulisho halali cha Taifa au kitambulisho kinachokubalika
  • Taarifa za benki kulingana na aina ya mkopo
  • Picha au nyaraka za dhamana pale zinapohitajika
  • Nyaraka za tender, LPO, au mkataba
  • BOQ au makisio ya gharama
  • Taarifa za benki za biashara
  • Usajili wa kampuni/biashara
Maswali

Maswali kuhusu Tender Loan

Tender Loan hutolewa kabla ya kazi kuanza?

Inaweza kutolewa baada ya tathmini ya mkataba, gharama, uwezo wa utekelezaji, na mpango wa malipo.

Nahitaji LPO au mkataba halisi?

Ndiyo. Nyaraka rasmi za kazi ni muhimu ili kuthibitisha thamani, muda, na chanzo cha malipo.

Marejesho yanawezaje kupangwa?

Marejesho yanaweza kuendana na cash-flow ya mradi au malipo ya mteja kulingana na tathmini ya GreenPath.

Ready to apply?

Anza maombi ya Tender Loan sasa.

Jaza fomu fupi ya mtandaoni kwa taarifa zako na kiasi unachohitaji. Timu ya GreenPath itawasiliana nawe kuthibitisha nyaraka, kutathmini uwezo wa marejesho, na kukuongoza katika hatua zinazofuata.

Anza maombi